1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Egon Bahr aaga dunia

20 Agosti 2015

Mwanasiasa wa chama cha Social Democratic - SPD nchini Ujerumani Egon Bahr amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 93.

https://p.dw.com/p/1GIMu
Deutschland Egon Bahr gestorben
Egon BahrPicha: picture-alliance/dpa/K. Schindler

Shirika la habari la Ujerumani limesema taarifa hizo zimethibitishwa na msemaji wa chama hicho. Bahr anatambulika nchini Ujerumani kama mjenzi wa siasa za Ujerumani ya mashariki.

Mwanasiasa huyo wa chama cha SPD mzaliwa wa jimbo la Thuringen alikuwa karibu mno na kansela wa kwanza wa chama cha SPD Willy Brandt.

Bahr alijadili pamoja na Urusi na Poland kuhusu mkataba wa kurejesha uhusiano wa kawaida na nchi hizo pamoja na kutoshambuliana.

Pia alishawishi mkaribiano kati ya iliyokuwa Ujerumani na magharibi na mashariki na uhusiano bora kati ya Ujerumani hizo mbili.

Baada ya kujizulu kansela Brandt mwaka 1974, Bahr chini ya kansela Helmut Schmidt alikuwa waziri wa uhusiano wa kiuchumi na maendeleo.

Kiongozi wa Chama cha SPD Sigmar Gabriel amezungumzia kifo cha Bahr akiliambia gazeti la Ujerumani "Bild" kuwa Bahr alikuwa mwana Social Democrat aliyetekeleza sera za chama kwa ukakamavu mkubwa.

Alipenda sana sera za kigeni. Mwishoni mwa mwezi Julai alisafiri kwenda Urusi kukutana na Rais wa zamani wa Urusi Mikhail Gorbachev ili kuhimiza mahusiano ya karibu kati ya Urusi na Ujerumani, ambayo yameporomoka tangu kuanza kwa mzozo wa Ukraine.

Mwandishi:Sekione Kitojo/dpa
Mhariri:Iddi Sessanga