1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mzozo wazuka juu ya serikali ya mseto Kenya

11 Machi 2008

Makubaliano lege lege ya kushirikiana madaraka nchini Kenya ili kukomesha mgororo wa umwagaji damu uliozuka baada ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo yamepata pigo.

https://p.dw.com/p/DMMa

NAIROBI

Yamepata pigp hilo hapo jana kutokana na kuzuka kwa mzozo juu ya dhima ya waziri mkuu katika serikali ya mseto iliopendekezwa.

Rais Mwai Kibaki na mpinzani wake Raila Odinga walitia saini makubaliano hayo mwezi uliopita kukomesha machafuko ya kisiasa ambayo yamesababisha kuuwawa kwa takriban watu 1,000 na kugharimu sifa ya Kenya ya kuwa mojawapo ya taifa imara kabisa la demokrasia barani Afrika.

Makubaliano hayo ya kihistoria yatamuingiza Odinga kwenye serikali kwa kuanzisha wadhifa wa waziri mkuu kwa ajili yake.

Hapo jana chama cha Odinga cha ODM kimekataa taarifa yenye kufafanuwa muundo wa serikali ya mseto iliotolewa na mkuu wa utumishi serikalini Francis Muthaura.Msemaji wa chama hicho Salim Lone amesema taarifa hiyo inaleta wasi wasi ni ya fitina na tishio kwa makubaliano hayo.

Wakosoaji wanasema taarifa hiyo ya Muthaura inaonekana kudunisha dhima ya waziri mkuu kwa kusema kwamba makamo wa rais ataendelea kubakia kuwa msaidizi mkuu wa rais.

Bunge linatarajiwa kukutana leo hii kujadili muswada wa sheria kuidhinisha makubaliano hayo kuwa sheria na kurekebisha katiba ya Kenya ili kuyafanya makubaliano hayo kuwa halali.