1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Timur Ivanov akamatwa kwa madai ya rushwa, Urusi

24 Aprili 2024

Maafisa wa usalama wa Urusi wamemkamata Naibu Waziri wa ulinzi Timur Ivanov kwa tuhuma za rushwa. Taarifa fupi ya kamati ya uchunguzi imetaja kuzuiliwa kwake kutatokana na kupokea hongo " kwa kiwango kikubwa."

https://p.dw.com/p/4f7nW
Urusi| Timur Ivanov
Naibu Waziri wa ulinzi Timur IvanovPicha: Russian Defence Ministry/dpa/TASS/picture alliance

Kukamatwa kwa ghafla kwa mshirika wa waziri wa Ulinzi Sergei Shoigu, ambaye Putin alimpa jukumu la kupigana vita nchini Ukraine, kumeibua uvumi kuhusu  vita dhidi ya ufisadi uliokithiri miongoni mwa viongozi wakuu wa jeshi na umma.

Waziri wa Ulinzi wa Ukraine kuondolewa katika wadhifa wake

Ikulu ya Kremlin imesema kwamba rais Putin amefahamishwa, kuhusu madai yanayomkabili Ivanov, ambaye amehudumu kama naibu waziri tangu 2016, chini ya majukumu yake alihusika pia na usimamizi wa majengo, makaazi, ujenzi na mikopo ya nyumba. 

Iwapo atapatika na hatia, Ivanov anakabiliwa na kifungo cha miaka 15 jela. Hata hivyo wizara ya ulinzi haikutoa tamko lolote.