1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI: Mazungumzo ya amani ya Somalia yapangwa upya

2 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCwo

Serikali ya mpito ya Somalia na Muungano wa Kiislamu zinafikiria kuwa na majadiliano mapya kati kati ya mwezi huu wa Novemba baada ya mazungumzo kukwama nchini Sudan.Kwa mujibu wa duru ya kidiplomasia mjini Nairobi,mazungumzo hayo yanatazamiwa kufanywa tarehe 15 Novemba. Majadiliano ya amani kati ya pande hizo mbili yaliodhaminiwa na Umoja wa Afrika,Umoja wa Ulaya na Umoja wa Kiarabu yalitazamiwa kuanza siku ya Jumatatu katika mji mkuu wa Sudan,Khartoum.Uamuzi wa kuahirisha mazungumzo hayo ulizidisha hofu ya kuzuka vita katika Pembe ya Afrika.