1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nairobi. Viongozi wa upinzani wakabidhi nyaraka za uteuzi.

15 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CG1G

Viongozi wa juu wa upinzani nchini Kenya jana wamejiunga na wito uliotolewa na jeshi la polisi nchini humo wa kuwa na kampeni za amani katika uchaguzi wa rais wakati walipokuwa wakiwasilisha karatasi zao za uteuzi kwa ajili ya uchaguzi huo.

Waziri wa zamani wa mambo ya kigeni Kalonzo Musyoka na mgombea mwingine Raila Odinga wamesema wakati wakikabidhi karatasi zao kwa tume ya uchaguzi nchini Kenya zinazohitajika kwa ajili ya kukubaliwa kugombea kiti cha urais katika uchaguzi wa Desemba 27. Tutafanya kampeni kwa amani . Hatutaki ghasia , Odinga ameliambia kundi kubwa la wafuasi wake baada ya kukabidhi karatasi hizo. Ameongeza pia kuwa anawataka wapinzani wake kujizuwia na ghasia.