1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI : Wasomali wanaokimbilia Kenya waongezeka

7 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD5U

Idadi ya Wasomali wanaokimbilia nchini Kenya imeongezeka sana na inaweza kuuweka pabaya uwezo wa kutowa misaada wa mashirika ya misaada.

Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa limesema hapo jana takriban wakimbizi 2,000 wamewasili kwenye vituo viwili vya mpakani katika siku mbili zilizopita na kufanya idadi ya wakimbizi waliokimbilia Kenya mwaka huu kufikia zaidi ya 30,000.

Shirika hilo la wakimbizi la Umoja wa Mataifa limesema iwapo kiwango cha zaidi ya wakimbizi 1,000 wanaowasili kwa siku kitaendelea kutafanya rasilmali za mashirika hayo ziemewe mno.

Kuongezeka huko kwa wakimbizi hivi karibuni inaaminika kuwa kunatokana na wapiganaji wa Muungano wa Mahkama za Kiislam kuteka miji kadhaa katika Bonde la Juba na kuwapotezea makaazi maelfu ya Wasomali.