1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nairobi. Wasomali warejeshwa kwao.

21 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCZK

Kenya jana Jumamosi imewarejesha washukiwa 34 wanaofikiriwa kuwa ni wa kundi la mahakama za Kiislamu nchini Somalia, mwanasheria wa wane kati ya watu hao ameliambia shirika la habari la AFP.

Harun Ndubi, wakili anayewawakilisha watu wane waliorejeshwa nchini Somalia, amesema kuwa Kenya imewaamuru washukiwa hao kuondoka nchini humo lakini imekataa kutoa sababu.

Ndubi amesema kuwa hakuna hata mmoja kati ya wateja wake hao wane walikuwa ni raia wa Somalia licha ya kuwa uraia wa wengine 30 ulikuwa unajulikana.

Hakuna mtu aliyesema kwanini watu hao walikamatwa na pia kwanini walirejeshwa nchini Somalia ikitiliwa maanani kuwa hakuna sheria nchini Somalia, Ndubi ameliambia shirika hilo la habari.