1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nairobi. Wasomalia waenda katika mkutano wa amani.

29 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCy9

Kundi la muungano wa mahakama za Kiislamu lenye nguvu nchini Somalia na serikali dhaifu ya nchi hiyo wanaelekea katika mazungumzo ya amani wiki hii huku kukiwa na hali ya wasi wasi wa kutokea vita ambayo inaweza kuliingiza eneo hilo la pembe ya Afrika katika mzozo mkubwa wa umwagaji damu.

Duru ya tatu ya majadiliano ambayo yanasimamiwa na umoja wa nchi za Kiarabu inatarajiwa kuanza Jumatatu nchini Sudan, lakini wakati hali ikizidi kuwa mbaya wanadiplomasia wanakabiliwa na vikwazo vingi katika kuzileta pande hizo mbili pamoja.

Kila upande umeshutumu mwingine kwa kuvunja makubaliano ya hapo kabla na serikali inahofia kuwa mataifa ya Kiarabu yanapendelea upande wa muungano wa Waislamu, ambao wanaendelea kudhibiti maeneo mapya licha ya makubaliano ya hapo awali.