1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI-watu watatu wauwawa Kibera Nairobi

18 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCie

Watu watatu waliuwawa na wengine wengi kujeruhiwa hapo jana baada ya polisi kupambana na watu walikuwa wakishiriki mkutano wa kisiasa uliopigwa marufuku katika mtaa wa mabanda wa Kibera mjini Nairobi nchini Kenya.

Hata hivyo mkuu wa polisi jijini Nairobi Njue Njagi alisema hakuna ruhusa iliyotolewa kwa polisi wake kutumia risasi hai dhidi ya mkutano huo na kwamba uchunguzi unafanyika juu ya tukio hilo.

Lakini kwa upande wao polisi walisema walilazimika kuchukua hatua hiyo baada ya mtu mmoja kuwafyatulia risasi.

Polisi walipiga marufuku mkutano huo uliokuwa ukiongozwa na kiongozi wa zamani wa kundi haramu la Mungiki Ndura Waruinge anayepanga kugombea kiti cha ubunge dhidi ya Raila Odinga kwenye uchaguzi wa mwakani.

Polisi nchini Kenya imeonya kutokea kwa ghasia za kisiasa katika uchaguzi wa Desemba mwaka ujao ambapo rais Mwai Kibaki anatarajiwa kukabiliana na upinzani mkali kutoka kwa mawaziri aliowafurusha kazini mwaka jana.