1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI:Kenya kupewa dola milioni 57

12 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCAe

Shirika la Fedha Duniani IMF limetoa idhini kwa Kenya kupewa takriban dola milioni 57 baada ya kuiondolea masharti kadhaa yanayohusiana na fedha zilizoko nchini na kutangaza mali ya maafisa wa ngazi za juu serikalini.

Kulingana na shirika hilo Kenya imeimarisha sekta yake ya biashara kubwa tangu mwaka 2004 ambapo sera mwafaka za kudhibiti deni la nchi kuzingatiwa vilevile ongezeko la viwango vya fedha nchini.

Kulingana na mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Murillo Portugal hatua za hivi karibuni zilizochukuliwa na serikali zimeimarisha taasisi kadhaa na uwazi ila bado mengi yanapaswa kufanywa.

Mwaka jana shirika la IMF nma Benki ya Dunia zilichelewesha kutoa mamilioni ya dola ya msaada kwasababu ya madai ya kashfa za rushwa