1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NATO NA UWANACHAMA WA UKRAIN

4 Aprili 2008

Ukrain na Georgia bado haziwezi kuwa wanachama wa NATO wakati huu-sababu ni munda inaotia Russia-jirani yao.

https://p.dw.com/p/Dc2i
Scheffer (kulia) na rais wa ukrain(kushoto)Picha: AP

Shirika la ulinzi la magharibi-NATO-katika mkutano wake mjini Bukarest,Rumania liliziahidi nchi 2 za zamani za kisoviet:Ukraine na Georgia kuwa siku moja zitakuwa wanachama wa NATO lakini kwa sasa, hazikukuingizwa katika utaratibu wa uanachama.Mojawapo ya sababu ni kuwa Russia ingali inapinga uanachama wa nchi hizo mbili.

Kwa upande mwengine, NATO na Russia zimeafikiana kutia saini mapatano yatayoiruhusu NATO kutumia njia za ardhini nchini Russia kusafirishia shehena na vifaavisivyo vya silaha kwa vikosi vya NATO viliopo nchini Afghanistan.

Rais wa Ukraine aneelemea kambi ya magharibi, alijaribu jana kuitoa wasi wasi russia kuwa juhudi za ukraine za kujiunga na shirika la ulinzi la NATO haziilengi Russia.Alisema hayo muda mfupi kabla kikao kati ya viongozi wa NATO na rais Wladmir Putin wa Russia .

NATO iliziahidi jana nchi hizo mbili Ukrain na Georgia wanachama wa zamani wa iliokua soviet union kwamba siku moja zitapewa uanachama huo zinaoutaka na hii zaidi yatokana na upinzani unaooneshwa sasa na Russia.

Viktor Yushcenko,rais wa ukrain amesema na nknamnukulu,

"Nchi yetu ina haki kamili kuchagua njia wetu wenyewe ya maendeleo,kutetea usalama na masilahi yetu.Masilahi yetu hayakusudii kwenda kinyume na nchi yoyote nyengine."

Katibu mkuu wa NATO Jaap de Hoop Scheffer kwa mara nyengine tena ameihakikishia Ukrain kwamba itafunguliwa njia ya kuelekea uanachama.Amesema kwamba hii ni ishara kutoka NATO kwamba inathamini usuhuba huo.

Ufaransa imeridhia kuchangia vikosi kwa Afghanistan,hatua ambayo imeiridhisha Kanada .Kanda ilitoa sharti ya kubakisha vikosi vyake huko tu ikiwa wanachama wengine wa NATO watachangia majeshi.

Rais Bush alielewa hapo kabla msimamo wa Ujerumani yenye vikosi Afghanistan lakini ina shida kuvitanua hadi kusini mjwa nchi hiyo ambako mapigano yna watalibani yamepamba moto.

Katibu mkuu wa NATO De Hoop Scheffer hapo amesema:

"Hapa Bukarest tumechora njia ya ramani tunakoelekea kwa azma moja ilio wazi:Kuanza awamu ya mpito ambamo serikali ya Afghanistan na wananchi wake wataifuata kwa usalama wao ."

Nae Kanzela Angela Merkel akichangia juu ya mada hii alisema:

"Sijatanabahi kuwa jana baada ya chakula chetu cha jioni tuliweza haraka kuafikiana kile ambacho ni cha msingi kwa mkutano huu wa kilele wa NATO.Nacho yale yanayounganisha pamoja shirika hili yamewekwa usoni kabisa.Na naamini kila kitu sawa."

Katika tokeo jengine muhimu mjini Bukarest,Russia na NATO zitatia saini makubaliano ambayo kwayo NATO itaruhusiwa kusafirisha kupitia ardhi ya russia vifaa na shehena zisizo za kijeshi kulishia vikosi vyake viliopo nchini Afghanistan.Ruhusa ya safari za anga ,haikutolewa kwa sasa na Russia.

Katibu mkuu wa NATo amesema mwezi uliopita kwamba ana matumaini ya kuongezeka kwa ushirikiano kati ya NATO na Russia.

Rais George Bush atakutana na rais anaeondoka wa Russia Wladmir Putin mwishoni mwa wiki hii huko Sochi,Russia.