1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nawaz Sharif arejea nyumbani.

26 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CTHf

Islamabad. Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Nawaz Sharif amerejea nchini humo kutoka uhamishoni nchini Saudi Arabia . Sharif na ujumbe wake walivamiwa na wafuasi wao baada ya ndege yake kutua mjini Lahore. Jaribio la kwanza la waziri mkuu huyo wa zamani kurejea kutoka uhamishoni alikoishi kwa muda wa miaka saba , lilishindwa miezi miwili iliyopita wakati rais Pervez Musharraf alipoamuru arejeshwe alikotoka kiasi cha saa chache tu baada ya kurejea. Mara hii jenerali Musharraf amesema kuwa Sharif hatakamatwa. Hata hivyo , mwanasheria mkuu wa serikali ya Pakistan ameripotiwa akisema kuwa Sharif huenda akazuiwa kugombea katika uchaguzi mkuu kwa kuwa amehukumiwa kifungo cha maisha kabla ya kwenda kuishi uhamishoni mwaka 2000. Hata hivyo Nawaz Sharif amesema kuwa amerejea nchini humo kushiriki katika uchaguzi.

Wakati huo huo , waziri mwingine wa zamani , Benazir Bhuto , ameripotiwa kujaza fomu za uteuzi kwa ajili ya uchaguzi wa bunge mwezi Januari. Alirejea nchini Pakistan mwezi uliopita.