1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nchi tisa zaidi zaongezeka katika umoja wa Schenge

21 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CeOd

BRUSSELS.Kuanzia leo Umoja wa Ulaya katika masuala ya uhamiaji yaani Schengen umepanuka baada ya nchi tisa mpya kuingizwa.

Nchi hizo ni pamoja na Estonia, Poland, Jamuhuri ya Czech, Hungary na Slovenia.Wakaazi wa hizo sasa wanaweza kuingia katika nchi nyingine wanachama wa umoja huo bila kizuizi chochote mpakani.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani Wolfgang Schäuble akizungumzia hatua hiyo ya kihistoria , amesema kuwa Ulaya iliyogawanyika sasa ni historia.

Viongozi wa Ujerumani na Poland asubuhi hii wataudhuria sherehe za ishara ya kufunguliwa kwa mipaka hiyo.