1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ndege ya Ethiopia yapata ajali ikielekea Nairobi

Saumu Mwasimba
10 Machi 2019

Ndege hiyo iliyokuwa ikitokea mjini Adis Ababa ilikuwa imebeba abiria 149 na wafanyakazi wanane imepata ajali asubuhi leo Jumapili

https://p.dw.com/p/3Ejkw
Ethiopian Air Lines
Picha: Ethiopian Air Lines

Ndege ya shirika la ndege la Ethiopia imeanguka leo asubuhi majira ya saa mbili na dakika arobaini na nne kwa saa za Afrika Mashariki  ikiwa na abiria 149 pamoja na wafanyakazi 8. Msemaji wa shirika hilo ambaye hakutowa jina lake  amethibitisha juu ya taarifa hiyo ambapo imetajwa ndege hiyo ilikuwa ikielekea mjini Nairobi nchini Kenya. Waziri mkuu wa Ethiopia ameandika katika ukurasa wake wa Twitta leo Jumapili,10.03.2019 ujumbe wa kutoa pole kwa familia za waliofiwa kufuatia ajali hiyo mbaya.Ingawa pia ujumbe huo haukutowa maelezo zaidi.Ujumbe umesema-

''Ofisi ya waziri mkuu kwa niaba ya serikali na wananchi wa Ethiopia tungependa kutowa pole zetu kwa familia zilizopoiteza wapendwa wao waliokuwa kwenye ndege ya shirika la ndege la Ethiopia aina ya Boeing 737 iliyokuwa ikielekea Nairobi Kenya asubuhi ya leo''

Ndege hiyo ilikuwa ikitokea jijini Adis Ababa. 

Mwandishi:Saumu Mwasimba

Mhariri:Sylvia Mwehozi