1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

N'DJAMENA:Kesi ya utekaji wa watoto kuhamishiwa mji mkuu

2 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C7AU

Mahakama kuu nchini Chad imeamua kuihamishia kesi ya utekaji wa watoto 103 wa Kiafrika katika mji mkuu badala ya mji mdogo ulioko mashariki mwa nchi hiyo.Watu 17 wanaozuiliwa kwa kuhusika katika njama hiyo wanashtakiwa kwa utekaji na watahamishwa kutoka Abeche hadi mji mkuu wa N’djamena katika siku chache zijazo.Kundi hilo linajumuisha raia wa Ufaransa,Uhispania na Chad ambao ni waandishi wa habari,wahudumu wa ndege na wafanyikazi wa shirika la msaada kwa watoto Zoe’s Ark.

Shirika hilo lilizuiwa wiki jana kuwasafirisha watoto hao kutoka Chad hadi Ufaransa ambako walipanga kuwahifadhi katika jamii za kuwalea ili kuepuka ghasia za Darfur.

Kulingana na Shirika la Umoja wa mataifa linalohusika na watoto UNICEF watoto hao walikuwa si yatima kamam ilivyodaiwa na Shirika la Zoes Ark.

Wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa inashuku madai ya shirika hilo la Zoe’s Ark kuwa watoto hao ni mayatima kutoka eneo la Darfur.