1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Netanyahu afuta mkutano na waziri wa nje wa Ujerumani

Oumilkheir Hamidou
25 Aprili 2017

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amekataa kumpokea waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Sigmar Gabriel. Kisa hicho kinatishia kuukorofisha uhusiano kati ya Ujerumani na Israel ambao tokea hapo ni tete.

https://p.dw.com/p/2btwc
Israel vervollständigt seine Raketenabwehr mit «David's Sling»
Picha: Reuters/A. Cohen

 

Kivuli kimetanda katika ziara ya waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Sigmar Gabriel nchini Israel. Waziri mkuu Benjamin Netanyahu ameufuta kwa ghafla mkutano wake pamoja na waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Sigmar Gabriel uliokuwa ufanyike mjini Jerusalem. Chanzo ni mjadala ambao mwanasiasa huyo wa kutoka chama cha Social Democratic alipanga kufanya na wawakilishi wa mashirika yanayoikosoa serikali na hasa wale wanaolaani ujenzi wa makaazi mepya ya wayahudi katika ardhi za wapalastina. Kwa siku kadhaa sasa Netanyahu amekuwa akielezea upinzani wake dhidi ya mjadala kama huo. Sigmar Gabriel lakini alikuwa akiutetea mjadala huo na kusema ni jambo la kawaida na ambalo wanalifanya katika nchi nyingi tu za dunia. Katika mahojianao na kituo cha televisheni cha ZDF, Sigmare Gabriel alisema leo asubuhi ikiwa Netanyahu atakataa kuzungumza nae basi hali hiyo ingawa itamhuzunisha lakini haitobadilisha chochote katika uhusiano wake na Israel. Mazungumzo yake na wapinzani wa serikali yataendelea kama ilivyopangwa baadae  mjini Jerusalem. Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani amepanga pia kukutana na rais wa Israel.

Waziri wa nje wa Ujerumani Sigmar Gabriel
Waziri wa nje wa Ujerumani Sigmar GabrielPicha: picture-alliance/dpa/B. von Jutrczenka

Uamuzi wa Netanyahu wakosolewa na wanasiasa mbali mbali Ujerumani

Mwenyekiti wa kundi la wabunge wa Ujerumani na Israel katika bunge la shirikisho Bundestag, Volker Beck wa chama cha walinzi wa mazingira die Grüne amemkosoa sana Netanyahu akisema "waziri mkuu wa Israel hawezi kuwawekea masharti wanasiasa ya nani  wazungumze naye na nani hafai.

Kiwingu kimetanda katika uhusiano kati ya Ujerumani na Israel. Serikali kuu ya Ujerumani ilikosowa mwezi february mwaka huu sheria iliyopitishwa nan Israel ya kuhalalisha makaazi 4000 ya wahamiaji wa kiyahudi katika ardhi za wapalastina. Muda mfupi baadae mashauri yaliyokuwa yamepangwa kufanyika mwezi unaokuja wa may kati ya serikali ya Ujerumani na ile ya Israel yakaakhirishwa-kwasababu ya ratiba. Hata hivyo vyombo vya habari vya Israel vilidai sababu halisi inatokana na kukasirishwa Ujerumani na sera za Israel za ujenzi wa makaazi ya wayahudi katika ardhi za wapalastina.

Waziri wa nje wa Ujerumani azungumza na waziri mkuu wa utawala wa ndani wa Palastina
Waziri wa nje wa Ujerumani azungumza na waziri mkuu wa utawala wa ndani wa PalastinaPicha: Reuters/M. Torokman

Ufumbuzi wa madola mawili ndio njia pekee ya kumaliza mzozo wa mashariki ya kati

Akiendelea na ziara yake Mashariki ya kati,waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani ameyatembelea maeneo ya utawala wa ndani wa Palastina na kuzungumza na waziri mkuu Rami Hamdallah mjini Ramallah. Sigmar Gabriel amesema ufumbuzi wa madola mawili ndio njia pekee ya kuufumbua mzozo wa Mashariki ya kati.

 

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/dpa/

Mhariri:Yusuf Saumu