1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Netanyahu asitisha ujenzi katika eneo linalokaliwa na Walowezi wa Kiyahudi

30 Julai 2009

Waziri Mkuu wa Isreal Benjamini Netanyahu amesitisha mradi wa nyumba mia tisa za makazi katika eneo lenye mzozo la Mashariki wa Jerusalem.Hatua hiyo imetajwa kutokana na shinikzo la Marekani.

https://p.dw.com/p/J0Bb
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akiwa na Mjumbe Maalum wa Marekani Mashariki ya Kati George Mitchell.Picha: AP

Hatua hiyo iliyotangazwa na kituo kimoja cha Televisheni nchini Israel mapema leo baada ya mzungumzo ya muda mrefu katika ya Uongozi wa Israel na Ujumbe Maalum wa Marekani Kushughulikia amani Mashariki ya Kati uliyo chini ya George Mitchell.

Nyumba hizo zilipangwa kujengwa katika kitongoji cha Pisgat Ze'ev moja katika maeneo ya Wapalestina yanayokaliwa na Walowezi wa Kiyahudi.

Palestna yenyewe inataka Eneo la Jerusalem ya Mashariki kurejeshwa katika imaya yao ili liwe makao makuu ya taifa lao tarajiwa.

Tofauti na Mtangulizi wake Waziri Mkuu Ehud Olmet hakufanya siri kutekeleza mpango wake wa kuendelea na ujenzi katika eneo la Israe linalokaliwa na walowezi wa kiyahudi na Mashariki mwa Jerusalem lakini Netanyahu alirejesha maeneo yanayokaliwa na Waarabu katika himaya ya Palestina.

Israel iliteka iliteka eneo la Mashariki ya Jerusalem pamoja na miji mingine yenye Kiyahudi,Kiislamu,Kikristo na Armenia pamoja na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan wakati wa vita ya Mashariki ya Kati ya mwaka 1967.

Wakati huo huo leo hii Jeshi la Israel limetaka kufanyika uchunguzi wa vitendo 14 vya kihalifu vinavyodaiwa kufanywa na Majeshi ya Israel katika vita vya Ukanda wa Gaza mwisho mwa mwaka jana.

Taarifa hizo zilizotolewa na Gazeti la kila siku la nchi hiyo linmaloitwa Jerusalem Post.

Limeeleza kuwa malalamiko karibu mia moja yalitolewa na vyanzo tofauti ikijumuisha,Wanaharakati wa Haki za Binadamu,Wapalestina pamoja na Wanajeshi walioshiriki operesheni iliyodumu kwa siku 22 katika maeneo ya Gaza.

Awali Jeshi la nchi hiyo halikukubaliana na ripoti iliyotolewa na Mamlaka ya Palestina iliyosema Wapalestina 1400,Waisrael 13 waliwawa katika mapigano hayo yaliyoanza Mwezi Desema mwaka jana na kumalizika Januari mwaka huu.

Miongoni mwa Waliyouwawa walikuwemo raia wa Palestina 926 pamoja na watoto 313.

Shirika la haki za Binadamu la Amnesty International lililaani vikali mashambulizi hayo ambayo yalitekelezwa na majeshi ya Israel kwa kuvurumisha makombora ya angani na ardhini katika makazi ya raia wakipalestina.


Mwandishi-Sudi Mnette DPAE

Mhariri.M. Abdul-Rahman.