1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Mbaroni kwa njama za kuripua uwanja wa JFK

3 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBvP

Watu wanne akiwemo mbunge wa zamani wa bunge la Guyana wamekamatwa kuhusiana na njama dhidi ya shughuli za uwanjani katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa John F. Kennedy mjini New York.

Maafisa wa serikali ya Marekani wamesema hapo jana kwamba watu hao wanne wamefunguliwa mashtaka ya kula njama za kuushambuli uwanja wa ndege huo wa JFK kwa kutega mabomu ya kuripuwa mapipa makubwa ya mafuta ya ndege na mabomba ya mafuta uwanjani hapo.

Mmojawapo wa watuhumiwa ni mfanyakazi wa zamani wa mizigo katika uwanja huo wa ndege.

Maafisa wa usalama wamesema uchunguzi wao umesaidiwa na mchongezi wa polisi ambaye alirikodi mazungumzo na watuhumiwa.