1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York. Mkutano wa mawaziri wa baraza kuu wamalizika.

4 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Im

Mkutano wa kila mwaka wa ngazi ya mawaziri katika baraza kuu la umoja wa mataifa umemalizika mjini New York , kwa wito wa kuchukuliwa hatua duniani kote kuhusiana na mabadiliko ya hali ya hewa, umasikini na ugaidi.

Rais wa baraza hilo Srgjana Kerim , waziri wa zamani wa mambo ya kigeni wa Macedonia , amesema kuwa karibu viongozi wa nchi 100 walishiriki katika mjadala wa kisiasa katika kikao cha 62 cha kila mwaka cha baraza hilo la mataifa 192, kilichoanza Septemba 18. Kikao hicho , ambacho kinaendelea hadi Septemba mwakani , kitakuwa kinajadili hatua za mageuzi , haki za binadamu na mipango ya umoja wa mataifa kama misaada ya kiutu na maendeleo katika miezi ijayo.