1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Somalia inahitaji msaada wa dharura

22 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBzf

Umoja wa Mataifa umetoa mwito kwa jumuiya ya kimataifa kutowasahau watu wa nchini Somalia. Mratibu wa misaada ya kiutu wa Umoja wa Mataifa, John Holmes alipozungumza katika Baraza la Usalama mjini New York alisema,nchi hiyo inahitaji msaada wa dharura.Kwa upande mwingine, serikali ya mpito ya Somalia,imemtuhumu Holmes kuwa hakutathmini kwa kina hali ya maafa nchini Somalia.Kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa,kiasi ya watu 400,000 wameukimbia mji mkuu wa Somalia,Mogadishu kwa sababu ya mapigano ya hivi karibuni.