1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK:Nchi zenye nguvu duniani zashindwa kuafikiana juu ya Iran

20 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCho

Nchi zenye nguvu duniani hapo jana zimeshindwa kwa mara nyingine kuafikiana juu ya pendekezo la Umoja wa ulaya la vikwazo dhidi ya Iran kuhusiana na hatua yake ya kukataa kuachana na mpango wake wa Kinuklia.

Wajumbe wa nchi tano wanachama wa kudumu kwenye baraza la usalama la Umoja wa mataifa Uingereza,China,Ufaransa ,Urusi na Marekani pamoja na Ujerumani walikuwa na vikao visivyo rasmi hapo jana ambapo walipitia waraka wa mapendekezo hayo lakini walishindwa kufikia mwafaka juu ya vipengele viwili muhimu vilivyoko kwenye waraka huo.

Balozi wa Urusi kwenye Umoja wa mataifa Vitaly Chrkin amepinga kipengele kinachotaka kuwekewa kikwazo cha usafiri maafisa 12 wanaohusishwa moja kwa moja na mpango wa kinuklia wa Iran unaoshukiwa na mataiafa ya magharibi kuwa wakutengeneza silaha za kinuklia.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Sean McCormack amelishinikiza baraza hilo la usalama la Umoja wa mataifa kupiga kura juu ya vikwazo hivyo kabla mwishoni mwa wiki.

Lakini kwa upande wake rais wa Iran Mahmoud AhmedNejad ameapa hapo jana kwamba nchi yake itachukua hatua ambazo hakuzitaja endapo baraza hilo la Usalama litaiwekea vikwazo hivyo.