1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nigeria yaadhimisha miaka 50 ya uhuru

Josephat Nyiro Charo1 Oktoba 2010

Kundi la waasi wa MEND wa Nigeria wametahadharisha kuwa watawashambulia kwa mabomu watu wataokohuhduria sherehe za leo

https://p.dw.com/p/PRrZ
Bango linaloonyesha Nigeria imetimiza miaka 50 ya uhuruPicha: Katrin Gänsler

Nigeria leo inatimiza miaka 50 tokea ilipopata uhuru wake mwaka 1960.Nchi hiyo iliyoko magharibi mwa Afrika, ni miongoni mwa nchi zenye nguvu kubwa kiuchumi barani humo.Na wakati nchi hiyo ikiadhimisha miaka hiyo 50 ya uhuru wake kundi moja maarufu la wanamgambo katika eneo la Delta nchini humo limeonya kutokea kwa milipuko.Hata hivyo kama alivyonifahamisha Katibu Mkuu wa zamani wa uliyokuwa umoja wa nchi huru za kiafrika OAU Dr Salim Ahmed Salim Nigeria imebakia kuwa nchi muhimu kwa bara la Afrika na wananchi wake kwa ujumla.

Mwandishi:Aboubakary Liongo

Mhariri:Josephat Charo