1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
AfyaNigeria

Nigeria yasema hakuna rekodi ya vifo kutokana na dawa ya J&J

17 Aprili 2024

Mdhibiti wa dawa nchini Nigeria amesema hakuna rekodi yoyote ya watoto waliokufa au kuugua kutokana na kuathiriwa na aina ya dawa ya kikohozi iliyotengenezwa na kampuni ya Johnson & Johnson ya huko Afrika Kusini.

https://p.dw.com/p/4esY1
Hakuna watoto waliokufa au kuugua Nigeria kutokana na kuathiriwa na aina ya dawa ya kikohozi iliyotengenezwa Afrika Kusini
Hakuna watoto waliokufa au kuugua Nigeria kutokana na kuathiriwa na aina ya dawa ya kikohozi iliyotengenezwa Afrika KusiniPicha: Colourbox

Mamlaka ya Kitaifa ya Usimamizi na Udhibiti wa Chakula na Dawa nchini Nigeria (NAFDAC) ilitangaza marufuku ya kutumia dawa hiyo baada ya vipimo vya maabara kugundua viwango vya juu na visivyokubalika vya kemikali aina ya "diethylene glycol", ambayo ni sumu kwa binadamu.Hatua hiyo ilipelekea nchi nyengine tano za kiafrika ambazo ni pamoja na Afrika Kusini, Kenya, Tanzania, Rwanda na Zimbambwe kuchukua uamuzi kama huo. Kutumia dawa hiyo ya kikohozi yenye kemikali hiyo huweza kusababisha matatizo ya figo na dawa hiyo tayari imesababisha makumi ya vifo vya watoto katika mataifa ya Gambia, Uzbekistan na Cameroon.