1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nini maana ya bure-bilashi na balaa-belua?

29 Juni 2011

Mtaalamu wa lugha wa Idhaa ya Kiswahili ya Deutsche Welle, Othman Miraji, azungumza na wataalamu wa lugha ya Kiswahili kutoka vyuo vikuu mbalimbali vya Ujerumani juu ya maana na matumizi ya bure-bilashi, balaa na belua.

https://p.dw.com/p/RWS5
Fukwe za Mashariki ya Afrika, kwenye chimbuko la lugha ya Kiswahili.
Fukwe za Mashariki ya Afrika, kwenye chimbuko la lugha ya Kiswahili.Picha: picture alliance/dpa

Magdeline Wafula: "Bure-bilashi ni msemo unaomaanisha "bila sababu yoyote."

Omar Babu: "Bilashi yatokana na neno la Kiarabu "bilaa shain" maana yake bila kitu...."

Prof. Said Ahmed Khamis: "Tumeishi na Waarabu kwa miaka isiyopungua 2000. Ni jambo la kawaida kuwa na athari kubwa ya Kiarabu kwenye lugha na utamaduni wa Kiswahili."

Mtayarishaji/Muongozaji: Othman Miraji

Washiriki/Wataalamu: Omar Babu (Chuo Kikuu cha Cologne), Sauda Barwani (Chuo Kikuu cha Hamburg), Profesa Said Ahmed Khamis (Chuo Kikuu cha Bayreuth) na Magdaline Wafula (Chuo Kikuu cha Eldoret, Kenya)