1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nouakhchout. Mauritania wapiga kura katika uchaguzi mkuu wa rais leo.

11 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCKQ

Mauritania inafanya uchaguzi mkuu leo Jumapili kumchagua raia wa kiraia ili kuchukua nafasi ya utawala wa kijeshi ambao ulikamata madaraka katika mapinduzi yasiyo mwaga damu hapo 2005.

Wapo wagombea 19 wanaowania kiti cha urais na kama hakuna atakayepata zaidi ya asilimia 50 ya kura anazotakiwa ili kushinda, duru ya pili itafanyika hapo March 25.

Kiasi cha watu milioni 1.1 wanahaki ya kupiga kura katika uchaguzi ambao unaonekana kuwa huru katika muda zaidi ya nusu karne nchini humo. Kwa mara ya kwanza wapiga kura watamchagua rais wa katika hali ya uwazi na huru, bila ya kuingiliwa na serikali , kiongozi wa utawala wa kijeshi unaoondoka madarakani Ely Ould Mohamed Vall amesema katika mahoajino siku ya Ijumaa.