1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NUKUÁLOFA: Tonga itafanya mabadiliko ya kisiasa

17 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCs4

Serikali ya Tonga imekubali kufanya mageuzi ya kisiasa,kufuatia ghasia zilizotokea katika mji mkuu wa kisiwa hicho cha Pacifik ya Kusini. Uchaguzi huru uliopendekezwa kufanywa mwaka 2008 ni hatua ya kimapinduzi katika nchi ambako hadi hivi sasa mawaziri wengi huteuliwa na utawala wa kifalme.Machafuko yalizuka katika mji mkuu Nukuálofa,baada ya watu kukusanyika kwa maelfu, kulalamika juu ya ukosefu wa demokrasia nchini humo.