1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Obama afurahishwa na maafikiano ya kutosambaa silaha za kinuklia

Sekione Kitojo29 Mei 2010

Rais Barack Obama amefurahishwa na makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano wa umoja wa mataifa yanayohuzu kuzuwia kusambaa kwa silaha za kinuklia.

https://p.dw.com/p/NcW5
Rais Barack Obama akitembea kuelekea mahali anapozungumza na waandishi habari katika ikulu ya Marekani White House.Picha: AP

Rais Barack Obama amefurahishwa na makubaliano yaliyoafikiwa katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa, kuhusiana na mkataba wa kuzuia kusambaa kwa silaha za nyuklia. Hata hivyo Obama alipinga vikali, kile alichokitaja ni kuilenga Israel, katika mkutano uliopangwa kufanyika mwaka 2012, na kuyaleta pamoja mataifa yote ya Mashariki ya Kati, ili kuondolea mbali kitisho cha silaha za nyuklia katika Mashariki ya Kati. Mataifa matano yanayomiliki silaha za Nyuklia, na ambayo yametia saini mkataba wa kuzuia usambazaji wa silaha hizo, yalikubaliana kuchukua hatua zaidi kuzuia tishio la silaha za nyuklia duniani. Mataifa hayo yanayoongozwa na Marekani, Urusi, China, Ufaransa na Uingereza- yote yameridhia pendekezo la kupunguza zana zao za nyuklia. Hatua hii sasa inaiwekea mbinyo zaidi Israel, pamoja na India, Pakistan na Korea Kaskazini- mataifa matatu ambayo yamekataa kutia saini mkataba huo wa kusambaa kwa silaha za nyuklia.