1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Obama akosoa ushughulikiaji wa janga la virusi vya corona

Sekione Kitojo
17 Mei 2020

Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama amewakosoa viongozi wa nchi hiyo wanaoshughulikia janga la virusi vya corona akisema  janga hilo linaonesha maafisa wengi "hata hawajidai tu kuwa wanawajibika."

https://p.dw.com/p/3cLaL
Video Still Obama Unterstützung Kandidatur Biden
Picha: Getty Images

Obama  alizungumza  katika kile  kinachojulikana kama "Show Me Your Walk" toleo la HBCU," tukio la  masaa  mawili  kwa  wanafunzi wanaohitimu  kutoka  vyuo  ambavyo  kwa  kihistoria  ni  vya watu wenye  asili  ya  Afrika  na  vyuo vikuu  lililotangazwa katika  You Tube, Facebook na  Twitter. Matamshi  yake  yalikuwa  bila kutarajiwa  ya  kisiasa, kutokana  na  eneo lenyewe, na  kugusia kuhusu  matukio ya  hivi  sasa kupindukia  virusi  na  athari  zake  za kijamii  na  kiuchumi.

USA Präsident Obama und Vizepräsident Biden
Barack Obama (kulia) na makamu wake wa zamani wa rais Joe BidenPicha: Reuters/J. Young

"zaidi  ya  kila  kitu, janga  hili  hatimaye limetoboa tena pazia  kwa ukamilifu  wake kuhusu  wazo  kwamba  watu  wengi  wanaohusika madarakani wanajua  kile  wanachokifanya," Obama  alisema. "Wengi  wao  hata  wanaonekani  kujidai  kuwa wanawajibika."

Baadaye  hiyo  jana, wakati wa  hotuba ya  pili  iliyotangazwa  katika televisheni, Obama alishutumu "kile kinachofahamika  kama  watu wazima, ikiwa  ni  pamoja  na  baadhi wenye vyeo vya juu  na  kazi muhimu" ambao  wanafanya "kile kinacholeta  hisia  nzuri, kile kinachoridhisha, kile  rahisi."

Obama  akosoa

"Ndio sababu  mambo  yanakwenda  ndivyo  sivyo," amesema.

Obama  hakumtaja  rais Donald Trump  ama  afisa mwingine  yeyote wa  serikali  kuu  ama  wa  kitaifa  katika  hotuba zake  hizo zote. Lakini  mapema  mwezi  huu , alimkosoa  vikali Trump katika  jinsi anavyolishughulikia  suala  la  janga  la  virusi  vya  corona kuwa ni "maafa  makubwa yenye mkanganyiko" katika  mazungumzo  ya simu na  wajumbe 3000 wa utawala  wake  iliyopatikana  na  Yahoo News.

Kombobild Barack Obama - Donald Trump
Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama(kushoto) na rais wa sasa wa Marekani Donald Trump

Matamshi  hayo  ya  kuanza  shule  ni  ishara  ya  hivi  karibuni kabisa  kuwa  Obama  ana  nia  ya  kuchukua  jukumu  kubwa  zaidi katika  uchaguzi unaokuja. Alikuwa  kimya  sana  katika  miaka  tangu alipoondoka  madarakani , hata  wakati  Trump  amekuwa akimshambulia. Obama  amewaambia  waungaji  wake  mkono  kwa njia ya  simu  kwamba  atakuwa "akitumia  muda  mwingi iwezekanavyo na  kufanya  kampeni  kwa  nguvu  kwa  kadiri ninavyoweza" kwa  ajili  ya  Joe Biden, ambaye  alikuwa  makamu wake  wa  rais.