1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Obama aongoza kwa uchunguzi wa kura za Iowa

3 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cjsv

DES MOINES Iowa

Kwa mujibu wa kura za uchunguzi Barak Obama wa chama cha Demokrat nchini Marekani amekuwa mbele kwa asilimia nne dhidi ya wagombea wenzaka John Edward na Hilary Clinton ikiwa ni masaa machache kabla ya wapiga kura kuwateuwa kuwania urais kwa tiketi ya chama hicho kwenye jimbo hilo la Iowa.

Obama na Edward wameweza kujimaarisha zaidi wakati wa usiku wakati Hilary Clinton ameshuka kwa pointi nne na kushika nafasi ya tatu ikiwa matokeo yatakuwa hivyo Mama Clinton ambaye alikuwa mstari wa mbele mgombea wa chama cha Demokrat atapata pigo kubwa.

Obama ana asilimia 31 ya kuungwa mkono akifuatiwa na Edward mwenye asilimia 27 na Clinton ana asilaimia 24.

Kwa upande wa chama cha Republican Mike Huckabee amejiimarisha kwa asilimia sita kwa kufikia asilimia 31 dhidi ya gavana wa zamani wa Masachuhusetts Mitt Romney.

Seneta wa zamani wa Tenessee Fred Thomson anashika nafasi ya tatu kwa kuwa na asilimia 11.