1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

OBAMA ATEULIWA RASMI.

Mtullya, Abdu Said28 Agosti 2008

Wajumbe kwenye mkutano wa chama cha Demokratik wamemteua seneta Barack Obama kukiwakilisha chama hicho katika kugombea urais wa Marekani.

https://p.dw.com/p/F6AD
Seneta Barack Obama.Picha: AP

DENVER.

Seneta  Barack  Obama ameteuliwa rasmi kuwa  mgombea  urais wa  chama cha demokratik.

Mgombea  mwenzi katika  wadhifa  wa makamu wa rais Joseph Biden  pia ameteuliwa  rasmi.

Obama  ni mwanasiasa wa kwanza mwenye asili ya kiafrika kukiwakilisha chama cha  demokratik katika kugombea urais nchini Marekani.

Aliteuliwa kwa kishindo  kwenye mkutano  mkuu wa  chama hicho unaofanyika mjini Denver, Colorado.

Hapo awali katika hotuba  ya kusisimua,aliekuwa mpinzani wake katika  kuwania nafasi hiyo, seneta Hillary Clinton alitoa mwito kwa wafuasi wake  wote wamwuunge mkono Barack Obama. Akihutubia wajumbe kwenye mkutano huo leo, naye aliekuwa rais wa Marekani  bwana Bill Clinton   ameahidi kufanya kila analoweza  kumuunga mkono Barack Obama.

Bill Clinton amesema  kuwa Obama yupo  tayari kuwa rais  wa Marekani.