1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Obama kuendelea na mpango wa kuwapa waasi silaha

Admin.WagnerD23 Julai 2013

Rais Barack Obama wa Marekani sasa ataweza kuendelea na mpango wake wa kuwapa silaha waasi wa Syria, baada ya wabunge wa bunge la Marekani kuondoa kikwazo baada ya baadhi yao kuwa na wasiwasi na mpango huo.

https://p.dw.com/p/19CJm
U.S. President Barack Obama speaks about the Trayvon Martin case in the press briefing room at the White House in Washington, July 19, 2013. REUTERS/Larry Downing (UNITED STATES - Tags: POLITICS)
USA Obama Reaktion Trayvon MartinPicha: Reuters

Akizungumza na  shirika la habari la Uingereza Reuters  hapo jana, mwenyekiti wa kamati ya uchunguzi ya baraza la wawakilishi Mike Rogers, amesema anaamini kwamba wapo katika nafasi ambayo inatao ridhaa kwa serikali ya taifa hilo kuendelea na mpango wake.

Mwezi Juni mwaka huu, Ikulu ya Marekani ilitangaza kuwa ingaliweza kutoa msaada wa kijeshi kwa makundi ya waasi wa Syria baada ya kuzuiwa kwa takribani miaka miwili iliyopita. Mmoja kati maafisa wa serikali walikuwa wakishuguhulikia mpango huo ambae alizungumza kwa masharti ya kutotajwa jina lake, amesema kwa muda mrefu wamekuwa wakijadiliana na bunge la Marekani ili kuweza kushughulikia vikwazo hivyo, na kwamba vyote vimetazamwa vyema kwa hivyo kwa sasa wataweza kuendelea nao.

Wasiwasi wa vyama vya siasa

Pande zote mbili za vyama vya Republicans na Democrats katika baraza la wawikilishi na bunge yaani Congress, kupitia kamati zao za uchunguzi zilionesha wasiwasi kwamba kitendo cha kuwapa waasi silaha kunaweza kufanya ziangukie katika mikono ya makundi ya wapiganaji wa kiislamu kama kile cha harakati za kundi la Al-Nusra. Vilevile itakuwa vigumu kufanya ulinganifu wa vita vya wenyewe kwa wenyewe na mapigano ya kumpinga rais wa taifa hilo Bashir a-Assad.

A Free Syrian Army fighter takes up a position as he points his weapon in Aleppo's Salaheddine neighborhood July 21, 2013. REUTERS/Ammar Abdullah (SYRIA - Tags: POLITICS CIVIL UNREST MILITARY CONFLICT)
Mpiganaji muasi katika mji wa AleppoPicha: Getty Images

Katika hatua nyingine mmoja kati ya majenerali wa juu kabisa katika jeshi la Marekani ameliarifu bunge la nchi hiyo kuhusu mpango wa kuingia kijeshi nchini Syria, lakini amesisitiza kwamba hatua hiyo inaweza kuwa kuingia vitani na mmoja wa kiongozi wa kiraia.

Mbunu za kukabiliana na mgogoro wa Syria

Katika barua yake iliyosambazwa hapo jana, mwenyekiti wa kamati ya pamoja ya viongozi hao Martin Dempsey ametoa mbinu tano za mbadala zikiwemo uchunguzi pasipo kutumia silaha kali na mafunzo yenye kuweza kuepusha madhara na kuondoa silaha za kikemikali nchini Syria.

Barua hiyo iliyotumwa kwa mwenyekiti wa kamati ya bunge la Marekani Carl Levin, vilevile imetaja hatari kama za kuyaongezea uwezo makundi ya wapiganaji ya kiislamu sambamba na mashambulizi ya kulipiza kisasi yanatakayofanywa na utawala wa Syria.

Umoja wa mataifa wasisitiza mazungumzo

Nae mjumbe wa amani wa Umoja wa Mataifa nchini Syria Lakhdar Brahimi amesema bado anaweka shinikizo kubwa katika mpango wa kufanyika mkutano wa amani, wenye lengo la kumaliza mapigano, pamoja na kutokuwepo kwa tarehe ya kufanyika mkutano huo mpaka sasa.

Akizungumza na waandishi habari nchini Marekani, Brahimi amesema si jambo rahisi kuwakutanisha pamoja watu ambao wamekuwa wakiuwana kwa miaka miwili mfululizo, litachukua muda lakini hatimae litaweza kufanikiwa.

Mjumbe huyo amesema Umoja wa Mataifa umeweka wazi kabisa kwa nchi ambayo ina maslahi kwa namna moja au nyingine inaweza kushiriki kuhudhuria mkutano huo ambao hivi sasa unatarajiwa kufanyika Septemba.

Mwandishi: Sudi Mnette/Afp Reuterss

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman