1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Obama kuongoza kumbukumbu ya mashambulizi ya September 11

Aboubakary Jumaa Liongo11 Septemba 2009

Rais Barack Obama hii leo anatarajiwa kuwaongoza wananchi wa Marekani katika kuwakumbuka kiasi cha watu elfu 3 waliyouawa katika shambulio la kigaidi la septemba 11 miaka minane iliyopita.

https://p.dw.com/p/Jcvz
Rais Barack ObamaPicha: picture alliance/dpa

Katika shambulizi hilo magaidi wa kundi la Al-Qaida waliziteka ndege nne za abiria za Marekani ambapo mbili walizibamiza na kulilipua jengo la kituo cha kimataifa cha biashara jijini New York, na nyingine  katika makao makuu ya Wizara ya ulinzi Pentagon Washington.

Rais Barck Obama anatarajiwa kutoa heshima kwa wahanga hao kwa kutoa hotuba katika makao makuu ya Wizara ya ulinzi Pentagon, kabla ya kukutana na ndugu na jama za watu waliyokufa katika shambulizi hilo.

Rais Obama atatembelea eneo la  Arlington, Virginia, ambako moja kati ya ndege hizo zilizotekwa, iliangukia katika makao makuu ya wizara ya ulinzi Pentagon, na kuwaua watu 184.

Ataongozana na Waziri wa ulinzi Robert Gates, pamoja na kiongozi wa wakuu wa majeshi ya nchi hiyo Michael Mullen.Eneo hilo la Pentagon ndiyo eneo rasmi la makumbusho ya mashambulizi hayo ya kigaidi.

US - Vizepräsident Joe Biden in Bagdad
Makamu wa Rais Joe BidenPicha: AP

Mjini New York, Makamu wa Rais Joe Biden, anatarajiwa kuhudhuria kumbukumbu hiyo katika eneo lilipokuwa kituo hicho cha kimataifa cha biashara ambalo sasa linajulikana kama Ground zero.

Siku ya kumbukumbu hiyo huanzia New York ambako ndege mbili zilijibamiza katika majengo ya kituo hicho cha kimataifa cha biashara na kuyateketeza, ambapo kiasi cha watu  2,700 waliuawa, wakiwemo askari wa kikosi cha zimamoto, wanajeshi na watu wengine wa  idara za uokozi.Kufuatia shambulizi hilo, Rais wa wakati huo George Bush alitangaza vita  dhidi ya ugaidi.

Katika eneo hilo la Ground Zero, ndugu na jamaa za watu waliyouawa katika shambulizi hilo, wanatarajiwa kuweka mashaada ya maua na kusoma majina ya wahanga hao.

World Trade Center Ground Zero Bauarbeiten
Ujenzi katika Kituo cha Kimataifa cha Biashara New York, ukiendeleaPicha: AP

Kazi ya ujenzi wa majengo mapya ambayo yamepewa jina la ´´Mara wa Uhuru´´.Kuna jengwa majengo matano marefu kabisa ambayo yatakuwa na eneo kubwa la bustan ya kupumzikia pamoja na kumbukumbu.Hata hivyo ujenzi wa majengo hayo umekuwa ukienda taratibu , na pia kukwazwa na mzozo wa kiuchumi dunia.

Huko Shanksville, Pennsylvania, ambako ndege ya nne iliyotekwa ilianguka katika eneo wazi, baada ya abiria kuwazidi nguvu watekaji, kumbukumbu ilianza jana kwa kusoma majina ya watu waliyokufa.

Wengi wanaamini kuwa watekaji hao walikuwa na nia ya kwenda kuibamiza ndege hiyo kwenye jengo la bunge la Marekani Capitol Hill mjini Washington.

Hapo siku ya Jumatano wabunge katika kikao chao huko Capitol Hill walitoa heshima zao kwa abiria waliyowazidi nguvu watekaji hao kwa kusema kuwa siyo tu kuwa waliweza kuokoa maisha ya watu wengi, lakini pia uharibifu mkubwa wa jengo hilo.

Mipango ya kumbukumbu ya tukio hilo huko Pennsylvania imekuwa ikukumbana na mgongano wa fikra na mawazo juu ya ujenzi wa makumbusho, ambapo kuna mijadala iwapo serikali itoe eneo binafsi kwa ajili ya ujenzi wa makumbusho hayo.

Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Marekani Colin Powell anatarajiwa kuhutubia katika kumbukumbu hiyo huko Pennsylvania.

Kwa wamarekani wengi kumbukumbu hii ni wakati  wa kukumbuka majeshi ya nchi hiyo yanayoendesha operesheni za kijeshi katika sehemu mbalimbali duniani, wakiwemo wale waliyopo Iraq na Afghanistan ambao walipelekwa mara baada ya azimio la vita dhidi ya ugaidi.

Msemaji wa Ikulu ya Marekani Robert Gibbs hapo jana alikiri kuwa Rais Barck Obama anajaribu kukwepa kutumia neno vita dhidi ya ugaidi, lakini akasema rais atawakumbuka  askari hao waliyoko katika maeneo mbalimbali duniani.

Mwandishi:Aboubakary Liongo/AFP

Mhariri:Mohamed Abdul-Rahman