1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Odinga ataka usaidizi wa nchi za Magharibi

Wakio10 Novemba 2017

Kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya NASA, Raila Odinga ameyaalika mataifa ya Magharibi kuhakikisha taifa la Kenya limeidhinisha demokrasia, baada ya uchaguzi mkuu uliogubikwa na utata.

https://p.dw.com/p/2nPTJ

Mwito huo umetolewa wakati Kanisa Katoliki nchini Kenya likiwa limetangaza litawaleta pamoja Raila Odinga na Rais Uhuru Kenyatta katika mazungumzo yatakayolenga kumaliza mzozo wa kisiasa ulioko nchini humo. Hata hivyo, hisia za kwamba taasisi za kitaifa zinakosa kuwa na uhuru wa kutekeleza shughuli zake ni jambo ambalo linatatiza juhudi hizi, hata kuibua mgawanyiko baina ya viongozi wa makanisa na wananchi kwa ujumla.  Kwa mengi zaidi msikilize mwandishi wetu kutoka Nakuru Wakio Mbogho.