1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Scholz na Xi wahimiza ushirikiano wa karibu kati ya nchi zao

John Juma
16 Aprili 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, amekutana na Rais wa China Xi Jinping, wakati wa ziara ya siku tatu katika nchi hiyo ya Asia na mshirika mkubwa wa kibiashara wa Ujerumani.

https://p.dw.com/p/4eqY3
Diplomasia | Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz akiwa na Rais wa China Xi Jinping.
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz akiwa na Rais wa China Xi Jinping.Picha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Mwanzoni mwa mkutano wao, Olaf Scholz na mwenyeji wake Jinping walitoa wito wa kuimarishwa kwa ushirikiano kati ya nchi zao.

Olaf Scholz aliangazia vita ndani ya Ukraine, ulinzi wa tabia nchi na ushirikiano wa kiuchumi. Alisisitiza kuwa vita vya Urusi dhidi ya Ukraine na silaha za nyuklia za nchi hiyo zitakuwa na athari mbaya kwa usalama wa Ulaya.

Soma pia:Scholz na Xi kujadili juu ya China kuisaidia Urusi kijeshi

Xi alisema kwa pamoja wanaweza kuimarisha utulivu na usalama zaidi ulimwenguni ikiwa watashikamana na kuzingatia kanuni za kuheshimiana, kutafuta mambo ya pamoja licha ya tofauti zao na kujifunza kutoka kwa kila mmoja.