1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Olmert kuzuru Ujerumani wiki ijayo

3 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D1jR

Waziri mkuu wa Israel, Ehud Olmert, atazuru mji wa Berlin kukutana na viongozi wa Ujerumani.

Olmert anatarajiwa kuwasili Jumapili ijayo hapa nchini kwa ziara ya siku tatu na atakutana na kansela Angela Merkel na rais Horst Kohler. Atalitembelea pia jumba la makumbusho la wayahudi mjini Berlin.

Viongozi hao watajadili maswala ya Mashariki ya Kati, changamoto za amani katika eno hilo, Iran na maswala muhimu kati ya Ujerumani na Israel.

Ujerumani ni mshirika mkubwa wa Israel barani Ulaya na inapinga juhudi za Iran kutaka kutengeneza silaha za nyuklia.

Pia ina idadi kubwa ya wanajeshi wake katika kikosi cha Umoja wa Mataifa kusini mwa Lebanon kilichotumwa baada ya vita vya mwaka juzi kati ya Israel na kundi la Hezbollah.