1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Operesheni ya Libya inayatimiza matakwa yetu asema Rais Obama

Thelma Mwadzaya29 Machi 2011

Rais Barack Obama wa Marekani ameielezea operesheni ya kijeshi ya Odyssey New Dawn inayoendelea nchini Libya kuwa harakati zinazoenda sanjari na matakwa ya kitaifa ya nchi yake.

https://p.dw.com/p/10jOZ
Rais wa Marekani Barack ObamaPicha: ap

Kiongozi huyo alisisitiza kuwa endapo hatua zisingechukuliwa,hilo lingeacha doa kubwa katika dhamiri ya ulimwengu.Rais Obama alieleza kuwa Jumuiya ya Kujihami ya NATO itaanza kuyatimiza rasmi majukumu yake nchini Libya hapo Jumatano (30.03.2011).Hata hivyo,Rais Obama aliahidi kuwa operesheni hiyo itachukua muda mfupi zaidi na gharama zake zitakuwa chache ikilinganishwa na vita vya Iraq.Kauli hizo zimetolewa muda mfupi kabla ya kikao cha kimataifa kitakacholijadili suala la Libya kuanza mjini London(29.03.2011).Mkutano huo utawaleta pamoja wawakilishi wa mataifa 35.Wakati huohuo,waasi wanaendelea na mashambulio yao yanayoelekea eneo la magharibi la Sirte anakotokea Kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi.