1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPakistan

Pakistan kufanya uchaguzi chini ya kivuli cha jeshi

6 Februari 2024

Kufungwa jela kwa waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Imran Khan na ukandamizaji wa chama chake cha Pakistan Tehreek-e-Insaf, kumetia dosari uchaguzi wa bunge unaofanyika kesho Februari 8.

https://p.dw.com/p/4c6VU
Pakistan
Wanasiasa wa Pakistan wakiwemo mawaziri wakuu wa zamani

Fikra za kawaida nchini Pakistan kuhusu uchaguzi mkuu wa kesho ni kwamba matokeo tayari yamepangwa. Wapakistan wengi waliozungumza na DW wanasema jeshi la nchi hiyo lenye nguvu, linatakakukiondoa chama chama Imran Khan cha Pakistan Tehreek-e-Insaf -PTI kushiriki uchaguzi huo kwa gharama yoyote.

Mkaazi mmoja wa Islamabad Aliya Durran alieleza kwamba hana mpango wa kura, kwasababu anamuunga mkono Imran Khan na hajaruhusiwa kushiriki uchaguzi.

Khan, ambaye inawezekana ni mwanasiasa mashuhuri nchini Pakistan, amezuiliwa kushiriki uchaguzi wa kesho. Amehukumiwa miaka mingi jela katika kesi tofautizinazohusiana na ufisadi na kuvujisha nyaraka za siri za serikali. Lakini utafiti wa kura za maoni unaonyesha kwamba chama chake cha PTI kinaongoza dhidi ya vyama viwili ambavyo ni hasimu wake mkuu.

Uchaguzi Pakistan | 2024
Kampeni za uchaguzi PeshawarPicha: Farid Ullah Khan/DW

Vyama hivyo ni kile cha Pakistan Muslim League(N) cha waziri mkuu wa mara tatu Nawaz Sharif na chama kingine cha Pakistan People's Party kinachoongozwa na Bilawal Bhutto-Zardari, mtoto wa kiume wa waziri mkuu wa zamani aliyeuawa Benazir Bhutto.

Soma: Kwanini Wapakistan hawajali kuhusu uchaguzi ujao

Harris Khalique ambaye ni katibu mkuu wa asasi isiyo ya kiserikali ya Tume ya Haki za Binadamu ya Pakstan anasema kwamba chama cha PTI, "bila shaka ndio chama maarufu" ndani ya taifa hilo. Anaendelea kueleza kwamba "kama uchaguzi ungefanyika katika mazingira huru na ya haki, chama cha PTI kitashinda viti vingi bungeni haswa katika miji mikubwa". Lakini anadokeza kwamba haoni kama watapata ushindi mkubwa.

Kutofautina kwa Khan na jeshi la nchi lenye nguvu

Mwaka 2018, wapinzani wa Khan walikuwa wameshutumu uanzishwaji wa kijeshi kama njia ya kumfungulia njia ya kusalia madarakani. Kura ya Aprili mwaka 2022 ya kutokuwa na imani naye, ilishuhudia Khan akiondolewa mamlakanina hapo ndipo mvutano baina yake na jeshi ulipoanza. Khan alilishutumu jeshi kwa kuratibu kura hiyo.

Pakistan
Chama cha PPP kikifanya kampeni PakistanPicha: PPP

Alidai pia kwamba Marekani ilishirikiana na jeshi na vyama pinzani vya kisiasa kumuondoa mamlakani, shutuma ambazo Washington ilizikana. Baada ya kukabiliana na jeshi kwa takribani mwaka mmoja, wafuasi wa Khan waliamua kuingia mitaani kote nchini kupinga kukamatwa kwake. Maandamano hayo yaligeuka kuwa ya ghasia, huku baadhi ya waandamanaji wakivamia vituo vya kijeshi na maeneo ya makaazi ya kijeshi.

Matukio hayo yaliyopachikwa jina la "ghasia za Mei 9" yalionekana kuwa kipimo cha mwisho kwa jeshi la nchi hiyo yenye idadi kubwa ya waumini wa Kiislamu na ishara ya uhusiano uliobadilika pakubwa.

Kampeni zakamilika: Kampeni za uchaguzi Pakistan kuhitimishwa leo

Katika miezi iliyofuata, mamlaka zilianza kuwafungulia mashitaka washukiwa wa maandamano wakiwemo wanachama wa PTI katika mahakama ya kijeshi. Kilichofuata ni kwamba maafisa wengi waandamizi na wa kati wa PTI waliamua kujiuzulu na kutangaza kuliunga mkono jeshi.

Pakistan inakwamaje kuondokana na siasa za matabaka?

Soma pia: Imran Khan ahukumiwa miaka 10 jela

Katika wiki za hivi karibuni, kumekuwa na ripoti za wagombeaji wa PTI kusimamishwa kuwasilisha karatasi za uteuzi na mahakama ya juu ikikataza chama hicho kutumia alama yake ya kipekee ya kriketi kwenye uchaguzi. Matukio hayo yamefanya uchaguzi wa kesho kugubikwa na utata mkubwa, huku wasaidizi wa Khan na baadhi ya wachambuzi wakidai kwamba kura hiyo tayari imeporwa kabla ya uchaguzi. Mwandishi wa habari Noreen Shams aliyeko Karachi anasema historia nzima ya Pakistan imegubikwa na uchaguzi "uliokwisha pangwa".

Nini kinafuata?

Uchaguzi wa kesho, hata hivyo, hauhusu tu umaarufu wa chama au mwanasiasa, yako mengi zaidi ya hilo. Pakistan inakabiliwa na mgogoro mkubwa wa kiuchumi, mfumuko wa bei, ukosefu wa ajira na majanga ya mazingira.

Kulingana na hali ilivyo, waziri mkuu wa zamani Nawaz Sharifanapewa nafasi ya kushinda uchaguzi wa kesho. Chama chake cha Pakistan Muslim League kinadai kwamba chama cha PTI hakipaswi kurejea mamlakani kutokana na hali mbovu ya kiuchumi na kisiasa.