1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pakistan: Musharraf kun'gatuka jeshini

15 Novemba 2007

Rais wa pakistan, jamadari Musharraf amepanga kun'gatuka kama mkuu wa majeshi kabla Desemba mosi.

https://p.dw.com/p/CIlg
Shinikizo la Musharraf limezidi
Shinikizo la Musharraf limezidiPicha: AP

Rais Pervez Musharraf wa Pakistan, atajiuzulu kutoka wadhifa wake wa mkuu wa majeshi kabla tarehe mosi ya mwezi ujao -aliarifu leo afisa wa hadhi ya juu serikalini huku Musharraf akiunda serikali yake ya mpito itakayo iongoza Pakistan katika uchaguzi mkuu Januari 9 mwakani.Kiongozi wa upinzani Benazir Bhutto nae amesema leo, Musharraf hakubaliki kama rais hata akivua mavazi yake ya kijeshi.

Tangazo kuwa Musharraf anapanga kujiuzulu kama mkuu wa majeshi kabla desemba mosi, limekuja wakati watoto 2 wakiume wameuwawa na ufyatuaji risasi wakati wa maandamano ya wafuasi wa kiongozi wa upinzani Benazir Bhutto.hivi ni vifo vya kwanza kabisa tangu jamadari Musharraf kutangaza hali ya hatari hapo nov.3.

Wakati huu jamadari musharraf ameshughulika mno na wasaidizi wake kuunda serikali mpya ya mpito kuiongoza Pakistan katika uchaguzi mkuu ulioahidiwa kufanya Januari,mwakani.Bunge la sasa lilivunjwa usiku wa manane hapo jana.

Jamadari Musharraf amekumbana na shinikizo kubwa ulimwenguni kumtaka avue mavazi ya kijeshi alioyan’gan’gania tangu kunyakua madaraka 1999,akomeshe utawala wa hali ya hatari na aruhusu uchaguzi huru na bila mizengwe.

Akiashiria kuacha madaraka makuu ya uongozi wa jeshi,jamadari Musharraf, anatazamia Mahkama kuu itakua imeshapitisha hukumu juu ya uhalali wa jamadari Musharraf wa kugombea tena ule wadhifa wa

Hapo kabla, Musharraf akisema anasubiri hukumu hiyo kabla hakuacha madaraka jeshini.

Wanaomkosoa wanadai kwamba wasi wasi wake juu ya hukumu hiyo itavyokua, ndio uliomuongoza kuitisha hali ya hatari Nov.3.

Taarifa karibu na Musharraf zasema serikali mpya ya mpito itaapishwa kesho ijumaa nah ii inafuatia kuvunjwa bunge hapo jana.

Viongozi wa vyama vya upinzani wengi wao ama wamo kizizini nyumbani au wamebidi kuishi uhamishoni nje ya nchi, wanazingatia kuususia kabisa uchaguzi ujao wakidai hautakua huru wala bila ya mizengwe chini ya hali ya hatari iliotangazwa.

Benzir Bhutto amezungumza kwa masaa 2 na balozi mdogo wa Marekani, Brian hunt alievuka waya za senyenge nje ya nyumba ya Bhutto ili kuonana nae huko Lahore.Hunt alikariri madai ya marekani kukomeshwa hali ya hatari na Musharraf kunÄ’gatuka kama mkuu wa majeshi kabla ya uchaguzi kuitishwa.

John Negroponte,makamo wa waziri wa nje Dr.c.Rice anatazamiwa kuwasili Pakistan kesho kushinikiza zaidi hofu za Marekani huku akimuona mshirika muhimu katika vita dhidi ya Al Qaeda na Taliban akipepesuka.

Mwanasiasa mwengine wa Upinzani stadi wa zamani wa cricket,Imran Khan, amehamishiwa Gereza kuu huko Lahore baada ya kushtakiwa chini ya sheria za ugaidi kwa kuwa tu alillalamika dhidi ya utawala wa hali ya hatari.