1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Bibi Royal atagombea urais nchini Ufaransa

17 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCs0

Kwa mara ya kwanza katika historia ya Ufaransa, mwanamke atagombea urais nchini humo.Chama cha Socialist kimemteua Segolene Royal,kugombea uchaguzi wa rais utakaofanywa mwaka 2007.Royal, aliekuwa waziri wa mazingira wa zamani,amepata zaidi ya asilimia 50 ya kura zilizopigwa na wanachama wenzake.Kwa hivyo hakutokuwepo duru ya pili dhidi ya waziri mkuu wa zamani Laurent Fabius na waziri wa fedha wa zamani Dominique Strauss-Kahn.April mwakani,Bibi Royal atapambana na Nicolas Sarkozy wa chama cha mrengo wa kulia kugombea wadhifa wa urais nchini Ufaransa.