1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS : Wafaransa wamchaguwa rais mpya

22 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC7y

Vituo vya kupiga kura vimefunguliwa nchini Ufaransa ambapo watu milioni 44 wanaostahiki kupiga kura leo wanamchaguwa rais mpya wa nchi hiyo.

Uchunguzi wa mwisho wa kura ya maoni umeonyesha mgombea wa sera za mrengo wa kulia Nicolas Sarkozy akiwa mbele kwa asilimia chache dhidi ya mgombea wa kisoshalisti Bibi. Segolene Royal akifuatiwa kwa karibu na mgombea wa sera za wastani Francois Bayrou na kiongozi wa sera kali za mrengo wa kulia Jean- Marie le Pen.

Iwapo kama inavyotarajiwa hakuna atakeyejipatia ushindi mkubwa wa uhakika wagombea wawili watakaongoza watarudia tena kuwania wadhifa huo hapo tarehe 6 mwezi wa Mei.

Uchaguzi huo wa kurithi nafasi ya Rais Jaques Chirac umekuwa ukidhibitiwa na masuala ya madeni ya serikali,ukosefu wa ajira na kutoridhika kijamii katika vtongoji vya wahamiaji.