1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Paris. Wagombea urais wamaliza kampeni zao, uchaguzi kesho.

21 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC8Y

Wagombea wa kiti cha urais nchini Ufaransa wamefanya mikutano yao ya mwisho ya kampeni kabla ya uchaguzi wa duru ya kwanza hapo Jumapili.

Mgombea anayeongoza Nicolas Sarkozy, kutoka chama cha kihafidhina cha UMP alijiunga na wanasoka nyota pamoja na mawaziri wakuu wa zamani katika mkutano wake mjini Marseille.

Danielle Mitterrand, mke wa rais wa zamani Francois Mitterrand , na waziri mkuu wa Hispania Jose Luis Zapatero walijitokeza kumuunga mkono mgombea wa chama cha kisoshalist , Segolene Royal katika mkutano wake mjini Toulouse.

Maoni ya hivi karibuni kabisa yanaonyesha kuwa Sarkozy ananafasi kubwa ya kusonga mbele katika duru ya pili hapo May 6 kama mmoja kati ya wagombea wawili watakaopata kura nyingi.

Royal anapambana na Francois Bayrou anayefuata mrengo wa kati katika nafasi ya pili. Zaidi ya mtu mmoja kati ya wapiga kura wa Ufaransa hawajaamua nani wa kumpigia kura.