1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Paris. Waziri mkuu wa Ufaransa amuunga mkono Sarkozy.

12 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCJn

Waziri mkuu wa Ufaransa Dominique de Villepin ametangaza rasmi kumuunga mkono mgombea wa mrengo wa kulia katika wadhifa wa urais , Nicolas Sarkozy.

Villepin , ambaye kwa muda mrefu amekuwa hasimu wa kisiasa wa Sarkozy ametangaza uamuzi huo katika mahojiano ya radio siku moja baada ya rais Jacques Chirac kutangaza kujiuzulu kutoka katika siasa katika hotuba aliyoitoa kwa njia ya televisheni.

Chirac anatarajia kung’atuka katika medani ya siasa May mwaka huu baada ya kufanyakazi kama mwanasiasa kwa muda wa zaidi ya miaka 40. Uchaguzi wa rais utafanyika katika duru mbili hapo Aprili 22 na May 6.

Uchaguzi unatarajiwa kuwakutanisha mgombea msoshalist Segolene Royal akipambana na Sarkozy pamoja na mgombea wa mrengo wa kati Francois Bayrou.