1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS:Olmert aendeleza kampeni dhidi ya Iran

23 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7DX

Waziri Mkuu wa Isreal Ehud Olmert leo anaenda Uingereza ambapo anatarajiwa kufanya mazungumzo na waziri Mkuu Gordon Brown juu ya mpango wa nyuklia wa Iran.

Bwana Olmert anatokea Ufaransa ambapo pia alijadili suala hilo na rais Nicolas Sarkozy. Waziri Mkuu wa Israel anataka Iran iwekewe vikwazo zaidi kutokana na mpango wake wa nyuklia.

Waziri Mkuu wa Israel pia ameshakutana na rais Vladimir Putin wa Urusi kuhusiana na Iran.