1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Real Madrid yasimama na Benitez

24 Novemba 2015

Rais wa Real Madrid Florentino Perez amemuunga mkono kocha Rafael Benitez, siku mbili baada ya klabu hiyo ya Uhispania kuduwazwa na mahasimu wao Barcelona magoli manne kwa sifuri

https://p.dw.com/p/1HB1D
Real Madrid Florentino Perez PK Pressekonferenz
Picha: picture-alliance/dpa/Lucapierregiovanni

Kichapo hicho kilizusha wito wa kuwataka Perez na Benitez wajiuzulu. Lakini baada ya mkutano wa bodi jana jioni, Perez amewaambia mashabiki kuwa anatarajia timu hiyo kuanza tena kushinda mechi zake haraka iwezekanavyo.

Aidha Perez amekanusha madai kuwa wachezaji wa Madrid wamemlalamikia kuhusu mbinu za kocha mpya, akisema kocha huyo ana uhusiano mzuri na wachezaji na uongozi wa klabu.

Ushindi huo mkubwa wa Barcelona dhidi ya Real Madrid siku ya Jumamosi katika mchezo wa EL Clasico nchini Uhispania ulisababisha mbinyo mkali kwa kocha Rafa Benitez baada ya kushindwa mara ya pili mfululizo katika La Liga na kuiweka timu hiyo kigogo cha soka nchini Uhispania pointi sita nyuma ya mahasimu wao makubwa Barcelona.

Atletico Madrid ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Real Betis na kuchupa hadi nafasi ya pili na pointi nne nyuma ya mabingwa watetezi Barcelona.

Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre/dpae/ afpe
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman