1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pigo kwa chama cha Republican nchini Marekani

Hamidou, Oumilkher11 Oktoba 2008

Sarah Palin alaumiwa kutumia vibaya wadhifa wake alipokua gavana

https://p.dw.com/p/FY3p

Washington:


Kamati ya utafiti wa maadili katika jimbo la Marekani la Alaska,limemkuta na hatia ya kutumia vibaya madaraka yake ya gavana, mgombea wadhifa wa makamo wa rais wa Marekani kwa tikiti ya chama cha Republican-Sarah Palin.Kamati ya bunge la jimbo hilo la Alaska imesema katika ripoti yake,Sarah Palin amemfukuza kazi afisa wa ngazi ya juu wa polisi,kwasababu za mvutano wa kibinafsi unaohusu familia yake.Sarah Palin anakanusha hoja hizo akisema ripoti hiyo imelengwa kisiasa.Kashfa hiyo inatishia kugeuka pigo kubwa kwa kampeni ya uchaguzi ya mgonbea kiti cha rais kutoka chama cha Republican,John McCain ambae utafiti wa maoni ya umma unaonyesha amepitiwa kwa pointi nyingi na mpinzani wake Barack Obama wa kutoka chama cha Democratic.