Polisi wauawa na wanamgambo nchini Irak
22 Novemba 2007Matangazo
Hadi watu 10 wameuawa kusini mwa mji mkuu wa Irak,Baghdad.Wanamgambo wanaoshukiwa kuhusika na al-Qaeda waliwaua polisi 8 waliokuwa wakipiga doria.Hapo kabla waliwapiga risasi wanajeshi 2 wa Kiiraki na kuwanyanganya gari lao.Wanamgambo hao walifyatua risasi katika mtaa wa Hawr Rajab kusini mwa Baghdad wanakoishi Wairaki wengi wa madhehebu ya Kisunni na ni ngome ya al-Qaeda. Viongozi wa makundi ya kikabila ya madhehebu ya Kisunni,wamekuwa wakiwajumuisha wanaume vijana katika vikosi vya polisi katika jitahada ya kuwatimua wafuasi wa al-Qaeda.