1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pope kumaliza ziara yake ya Marekani leo

20 Aprili 2008
https://p.dw.com/p/Dl4d

New York:

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani, Papa Benedikti wa XVI anamaliza ziara yake ya siku tano nchini Marekani akiwaalika watu 24 wenye mafungamano na kile kinachojulikana kama "Ground Zero" mahala palipotokea hujuma ya kigaidi katika jengo la kituo cha biashara duniani Septemba 11 , 2001 . Watu 2,700 waliuwawa katika shambulio hilo. Waalikwa hao 24 ni walionusurika, jamaa wa waliouwawa na wafanyakazi 4 wa shughuli za uokozi. Papa Benedikti ataomba amani, matumaini na uzima wakiwemo wanaoungua baada ya kuvuta hewa ya sumu kutoka kwenye vifusi vya jengo hilo.