1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PRAGUE: Marekani kushauriana na Jamhuri ya Czech kuhusu mitambo ya ulinzi

21 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCZB

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Czech, Mirek Topolanek amesema Marekani inataka kuanzisha mashauriano kuhusu eneo la ujenzi wa mitambo ya kiulinzi ya Marekani nchini humo.

Waziri Mkuu huyo amesema mradi huo utajumuisha pia ujenzi wa mtambo wa kuchunguza vyombo vya angani pamoja na makombora.

Marekani imewasilisha ombi rasmi kuhusu mashauriano hayo punde baada ya serikali ya Mirek Topolanek kuidhinishwa siku ya Ijumaa iliyopita.

Serikali hiyo mpya inaunga mkono mpango huo wa Marekani wa kujenga mtambo wa ulinzi.

Mradi huo unakabiliwa na upinzani mkali nchini humo.

Marekani inapanga kupeleka mitambo kadha ya kijeshi barani Ulaya kuimarisha ulinzi wake dhidi ya mashambulio inayohofia huenda yakatekelezwa na Korea Kaskazini au Iran.

Mabaraza yote mawili ya bunge la Jamhuri ya Czek yanatakikana kuidhinisha mpango huo.

Serikali inahitaji kura mia moja miongoni mwa kura za wabunge mia mbili wa baraza la chini.