1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kaskazini

Pyongyang yaonya kuhusu ushushushu wa washirika wa Marekani

Saleh Mwanamilongo
13 Mei 2024

Korea Kaskazini imewaonya washirika wa Marekani, ikiwa ni pamoja na Ujerumani, Ufaransa na Uingereza, kuacha kuchochea mvutano katika eneo la Asia-Pasifiki.

https://p.dw.com/p/4fn2O
Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un
Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un Picha: KCNA/AP Photo/picture alliance

Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kaskazini, leo Jumatatu, imelaumu uingiliaji kati kijeshi katika kanda hiyo, kwa kisingizio cha kufuatilia ukiukaji wa vikwazo vya Umoja wa Mataifa.Taarifa iliyotolewa na shirika la habari la Korea ya Kaskazini imezitaka Ujerumani, Ufaransa,Uingereza, Australia, New Zealand na Canada, kuacha mara moja uchochezi unaosababisha mvutano na ukosefu wa utulivu.

Korea Kaskazini imesisitiza kuwa itachukua hatua zinazohitajika kutetea mamlaka na usalama wa nchi yake.

Mvutano kwenye eneo hilo ni mkubwa. Mnamo mwezi uliopita, Marekani ilifanya luteka za kijeshi za siku mbili katika eneo la Asia-Pasifiki, zilizowahusisha wanajeshi wa Korea Kusini na Japan.