1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Qanajeshi walioasdi wasalim amri Philippines

Oummilkheir29 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CUhr

Manilla:

Serikali ya Philippines imetangaza sheria ya kutotoka ovyo katika mji mkuu Manilla kufuatia njama ya kundi dogo la wanajeshi wanaoasi ya kutaka kumpindua rais Gloria Arroyo.Sheria hiyo ya kutotoka ovyo inaanza saa sita za usiku hadi alfajiri.Kabla ya hapo askari jeshi 50 na polisi wa kijeshi walifanya fujo kwa muda wa saa sabaa.Walijifungia katika hoteli moja ya fahari mjini manilla na kuwatolea mwito wananchi waandamane dhidi ya rais Arroyo.Jeshi liliivamia hoteli hiyo na kuwakamata waasi.Kiongozi wao ni jenerali Danilo Lim anaehusika na njama kadhaa za mapinduzi ikiwa ni pamoja na ile iliyoshindwa ya mwaka 2003.